BUPIGU
WATUMIA VEMA MTO MTUMBISI
Badala ya kusubiri mvua
zinyeshe ndipo waingie mashambani,wakazi wa kijiji cha Bupigu wilayani Ileje
mkoa wa Songwe wamejiingiza katika kilimo cha umwagiliaji wakati wa kiangazi hali
inayowapunguzia makali ya maisha.
Uchunguzi uliofanywa na
mwandishi wetu umebaini juu ya uwepo wa mashamba madogo madogo ya mahindi, magimbi,
mpunga, miwa, mbogamboga, ufugaji samaki na utunzaji wa mazingira.
Wakulima hao walieleza kuwa
licha ya kunufaika na kilimo hicho kinachowapunguzia makali ya maisha kumekuwa na tatizo la soko kwa mazao
wanayozalisha hususani mbogamboga.
Kijana
akiwa kwenye shamba la magimbi lililo kandokando ya Mto Mtumbisi.
Shamba
la mahindi linalomwagiliwa Bupigu
Mama
na watoto wake wakiandaa shamba la mpunga
Uoto
wa asili aina ya makangaga uliotunzwa na kikundi cha Mkombozi
Mwanachama
wa kikundi cha Mkombozi akiwa karibu na bwawa lao
Uoto
wa asili wa kipekee katika kijiji hicho unaotunzwa vema usitoweke
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni