Katibu Tawala wa Wilaya ya Ileje akifungua kikao cha kupanga mikakati ya kupunguza maambukizi mapya ya VVU na UKIMWI.
WILAYA YA ILEJE YATAKIWA KUJIPANGA DHIDI YA VVU NA UKIMWI
Na;Daniel Mwambene: Songwe
Katika kupunguza maambukizi mapya ya VVU na UKIMWI makundi mbalimbali
wilayani Ileje yametakiwa kuchukua hatua za dhati katika kulikabiri janga hili
ambalo lilishatangazwa na Awamu ya Tatu.
Hayo yalisemwa na wawakilishi wa
makundi mbalimbali waliokuwa wakichangia kwenye kikao cha kupanga mikakati ya
kupunguza maambukizi mapya katika wilaya hiyo kilichofanyika kwenye ukumbi wa
halmashauri .
Mratibu wa TACAIDS mikoa ya
Songwe na Mbeya Emamanuel Petro akisoma taarifa ya UKIMWI kitaifa na kimkoa
aliwataka wajumbe hao kuwa na mkakati itakayokwenda sambamba na mikakati ya
kimkoa na kitaifa.
Henry Kayuni Mwenyekiti wa Muungano wa Vikundi vya WAVIU wilayani Ileje
aliwataka wananchi wote kujiepusha na unyanyapaa kwa wenye VVU na kuwataka watu
wenye maambukizi hayo kujitangaza ili kuiokoa jamii badala ya kujificha
wakiendelea kuambukiza.
Naye mwakilishi wa makundi ya
dini katika mafunzo hayo Shekh wa wilaya hiyo Khamiss Simbeye aliwataka wakazi
wa wilaya hiyo kushikilia mafunzo ya dini zao.
Mwenyekiti wa Kamati ya UKIMWI ya
Halmashauri ya Wilaya hiyo Mh.Diwani Gwalusako Kapesa aliwataka wanafunzi ambao
wapo majumbani baada ya shule kufunga wasitumie muda huo kujihusisha na vitendo
vya ngono kwa kutumia mwanya kuwa mbali na sheria za shule.
Akifunga mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi
wa halmashauri hiyo Najum Tekka aliwataka walimu wa shule za msingi na sekondari
kuunda klabu za mapambano dhidi ya UKIMWI.
Tangu serikali ianzishe Sera ya
UKIMWI ya mwaka 2001 maambukizi yamekuwa
yakipungua kutokana na mikakati inayotoa elimu kuanzia ngazi ya familia
hadi Taifa
Mratibu wa TACAIDS mikoa ya Songwe na Mbeya Emmanuel Petro
akiwezesha katika kikao hicho.
Kaimu Mkurugenzi Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Ileje Bi;
Nujum Tekka akifunga kikao hicho.