HOSPITALI YA WILAYA YA
ILEJE YAPATA MSAADA WA MASHUKA
Na;Daniel
Mwambene,Songwe
Katika kukabiliana na tatizo la uhaba wa vifaa
mbalimbali,hospitali ya Itumba imepokea mashuka 200 kutoka kwa mbunge wa Jimbo la Uchaguzi la Ileje ikiwa ni sehemu ya
mashuka 600 yatakayotolewa na mbunge
huyo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mashuka hayo, Katibu wa mbunge Deo Mulungu alisema kuwa mashuka
mengine 400 yatakabidhiwa mara
yatakapofikishwa jimboni humo siku chache zijazo ,hivyo kukamilisha jumla ya
mashuka 600.
Katibu huyo alieleza kuwa,mafanikio hayo yamefikiwa kutokana
na juhudi za Mh.mbunge katika kutafuta wadau mbalimbali walio tayari kuchangia
maendeleo ya wilaya hiyo.
Akipokea msaada huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya hiyo Haji Mnasi alipongeza juhudi
hizo na kuahidi kusimamia matumizi sahihi ya mashuka hayo na kuwapunguzia kero
wagonjwa amboa huhitaji faraja muda wote wawapo hospitalini.
Kaimu Mganga Mkuu wa
Wilaya hiyo Rowland Mroso akishukuru kwa niaba ya watumishi wa hospitali
hiyo aliahidi kutunza mashuka hayo kwa mujibu wa taratibu za afya na aliomba
kutochoka kutoa misaada pale mbunge huyo atakapoombwa tena.
Hata hivyo,bado hospitali hiyo inakabiliwa na matatizo lukuki
ikiwemo kukosa mtaalam wa kutumia
mashine ya x-ray ambayo ilishanunuliwa.
Tangu kupewa kibali cha kuwa hospitali ya wilaya wananchi wa tarafa ya Bulambya wamepunguziwa
kero ya muda mrefu ambapo hapo awali walilazimika kusafiri hadi hospitali ya
Isoko zaidi ya kilometa 60 au kwenda nchi jirani ya Malawi.
Kaimu Mganga Mkuu akimshurukuru Katibu wa Mh.Mbunge
Maboksi yenye mashuka 200 kwa ajili ya hospitali ya Itumba ambayo ni hospitali ya wilaya Ileje
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Haji Mnasi (kushoto) akiwa na Katibu wa Mh.mbunge(kulia) wakiwa katika
eneo la hospitali kabla ya makabidhiano ya mashuka yaliyotolewa na Mh.Janet
Mbene(mb).
Kaimu Mganga Mkuu Rowland Mroso (mwenye miwani) akishukuru kwa niaba ya watumishi wa hospitali hiyo na kuahidi kuyatunza vema.
Mkurugenzi akishukuru baada ya kupokea msaada huo akiahidi kusimamamia matumizi yake
Mmoja wa watumishi wa hospitali hiyo Oscar Kaponda
akishukuru kwa msaada huo na kuomba mbunge aendelee kutafuta wadau wanaoweza
kusaidia vifaa vingine vinavyopungua ikwemo ‘’utra sound’
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni