Jumatatu, 28 Novemba 2016
MAFUNZO YA USAJILI WA WATOTO WA CHINI YA MIAKA MITANO WA VYETI VYA KUZALIWA
Mafunzo ya utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa umri wa chini ya miaka mitano yaliyokuwa yanaendeshwa na wataalamu wa RITA kutoka makao makuu. Mafunzo haya yamefanyika tarehe 28/11/2016 katika ukumbi wa shule ya sekondari Itumba yakihusisha watendaji wa kazi zote 18 za Halmashauri ya Wilaya ya Ileje, wafanyakazi wa vituo vya afya na zahanati zote za serikali na binafsi katika wilaya ya Ileje.
Baada ya kutoa mafunzo wataalam hao waliweza kugawa simu moja moja kwa kila mtendaji wa kata na vituo vyote vya afya na zahanati isipokuwa kwa kata na vituo vya afya ambavyo havina mtandao wa Tigo.
Simu hizo zimesimikwa mfumo maalum wa RITA utakaotumika katika kufanya usajili wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wa chini ya miaka mitano.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni