Na
Danil Mwambene Ileje 15,November,2016 Msitu
Katika
kutekeleza maagizo ya viongozi wa ngazi za juu pamoja na kuwatumikia wananchi viongozi
wilayani Ileje wameacha kutumia muda mwingi kukaa ofisini na badala yake
kutembelea wananachi na kufika wenyewe sehemu ya matukio badala ya kusubri
kupokea taarifa mezani.
Katika kutekeleza haya Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bi. Mary Joseph Marco alitembelea msitu wa serikali uliopo kijiji cha Chilemba kata ya Lubanda ili kufuatilia uwepo wa magogo yaliyotelekezwa na watu waliokuwa wamevamia msitu huo ili kupasua mbao pamoja na uharibifu mwingine unaofanywa katika msitu huo.
Ziara hiyo ilifanywa ikiwa ni mfulululizo wa ziara zilizofanywa na viongozi wa wilaya hiyo akiwemo Mkuu wa Wilaya Bw.Joseph Modest Mkude.
Katika ziara hiyo kiongozi huyo alibaini mambo kadhaa ambayo kama angekaa ofisini kusubiri taaarifa za mezani asingeyaona.
Mambo hayo ni pamoja na kuvamiwa kwa msitu na baaadhi ya watu wakipanda miti isiyo rafiki wa maji huku wakikata miti ya asili na kuendelea kuingiza mipaka ya mashamba yao ndani yam situ bila kuchukuliwa hatua za kisheria na viongozi wa eneo hilo.
Pia Katibu Tawala huyo alijionea kilimo kisichozingatia utunzaji wa vyanzo vya maji ambapo wananchi wamekuwa wakilima ndani ya mita zinazokatazwa kisheria.
Mara baada ya ziara hiyo iliyochukua zaidi ya masaa mawili ndani yam situ huo kiongozi huyo aliwataka viongozi wa kijiji na kata hiyo wanabainisha majina ya watu waliopanda miti ndani yam situ wa serikali kwa manufaa yao binafsi.
Pia aliagiza miti yote isiyo rafiki wa maji iliyopandwa ndani yam situ inang’oliwa na taarifa ipelekwe ofisini kwake.
Aidha,aliagiza mikutano ya wananchi iitishwe ili kuelezwa sheria ya hifadhi ya madingira na athari za ukataji wa miti ya asili kwa kizazi hiki na kwa vizazi vijavyo.
Diwani wa kata hiyo Mh.Laisoni Pimba Ngabo aliahidi kushirikiana na viongozi wenzake pamoja na wananchi katika kurejesha mazingira yaliyohaibiwa kwa kuyalinda.
Mmoja
wa wajumbe wa Serikali ya kijiji Kibona alikiri juu ya uwepo wa uvamizi wa
msitu huo akisema wanafanya hivyo wakati wa vikao na usiku wakijua
ufuatiliajiunaweza kuwa mgumu.
Hivi karibuni Waziri January Makamba na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni mstaafu Chiku Galawa waliwataka viongozi wa wilaya ya Ileje kuchukua hatua za haraka katika kulinda mazingira kwa kusimamia upandaji miti unaolinda vyanzo vya maji.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni