SARE YAWANYIMA RAHA
MASHABIKI WA TIMU YA MWENGE
Na Daniel
Mwambene,Songwe
Ikiwa
inamalizia mchezo wake wa mwisho wa Ligi
Daraja la Tatu Mkoa wa Songwe
timu ya soka ya Mwenge Sports Club ya Ileje imeshindwa
kuwapa raha mashabiki wake baada ya kutoka suluhu na timu ya Vwawa Town
ya Wilaya ya Mbozi mkoani humu.
Ikiwa
katika uwanja wake wa nyumbani katika
kiijiji cha Isongole mbele ya Mkuu wao wa Wilaya Joseph Mkude Mwenge ilishindwa kutumia nafasi kadhaa ilizozipata
kutokana na umahili wa golikipa Michael Mwakatera wa timu ya Vwawa.
Licha
ya kufika mara kadhaa langoni mwa Vwawa kwa kuipenya ngome ya Vwawa iliyokuwa
ikongozwa na Juma Siame na Geofrey Kasebele, Mwenge ilishindwa kabisa kutikisa
nyavu za maadui huku mashabiki wake waliokuwa wamefurika kwenye uwanja
uliozungushiwa’ matrubai’wakiwa wamesimama kushangilia wakidhani kuwa lilikuwa ni goli.
Licha
ya kufanya mabadiliko kwa kila timu hadi dakika 90 zikikamilika si Mwenge wala
Vwawa waliokuwa wamepata goli.
Matokeo
haya yanaiwezesha Mwenge kufikisha pointi tisa kwenye kundi lake ikiungana na timu ya Morning Star ya Tunduma
wilayani Momba na timu za makundi mengine
ili kuingia katika hatua nyingine ya ligi ya mkoa huo
Akizungumza
mara baada ya mchezo huo mmoja wa mashabiki ya timu hiyo,Zakaria Kyomo alisema
kuwa mchezo ulikuwa mzuri ila ladhaa
yake ilipungua kutokana na kutopata goli.
Timu
hii ni mojawapo ya timu kongwe wilayani Ileje timu zingine ni pamoja na Itumba
Stars,Mbebe Rangers na timu ya Uhuru
toka kataLubanda.
Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ileje akiwasili uwanjani kwa ajili ya kushuhudia mechi
Wachezaji wa timu ya Vwawa wakipasha kabla ya mechi kuanza
Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ileje akiingia Uwanjani kushuhudia mchezo
Mh. Mkuu wa Wilaya Ileje alikagua wachezaji kabla ya Mechi kuanza
Mh. Mkuu wa Wilaya akitoa mawaidha kwa wachezaji kabla ya mchezo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni