Jumatano, 23 Novemba 2016

TIMU YA MWENGE YANG’ARA LIGI YA KITAIFA NGAZI YA MKOA WA SONGWE


Na ;Daniel Mwambene ,Ileje –Songwe

Wakati ligi Daraja la Tatu hatua ya awali ikielekea mwisho timu ya soka ya Mwenge Sports Club imezidi kung’ara baada ya kuibuka na pointi tatu ikiilaza IFAD ya toka wilaya mpya ya Songwe kwenye mchezo kipolo uliokuwa umekatizwa na mvua katika uwanja wa Vwawa ambayo  ni Makao makuu ya mkoa wa Songwe.
Mpaka sasa timu hiyo imefikisha pointi tatu ikiwa imecheza michezo minne ikishinda miwili na kutoa sare mechi mbili imefikisha pointi nane na kuongoza kundi lake lenye jumla ya timu sita.

Mwenyekiti wa timu hiyo,Bw Raymond Mlaga akizungumza wakati wa mapokezi ya timu yake alisema kuwa wamebakiza mchezo  mmoja dhidi ya Vwawa Town  utakaochezwa katika uwanja wao wa nyumbani wa Mwenge na aliwaomba mshabiki kujitokeza siku ya Jumapili  ijayo kuishangilia timu yao ya Mwenge ili iibuke na ushindi.


Picha za hapa chini na mapokezi ya timu ya Mwenge ikiwasili wilayani Ileje ikitokea Vwawa 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni