MKOA WA SONGWE
KUVALIA NJUGA SEKTA YA ELIMU
Na;Daniel Mwambene, Songwe
Wakati ya kitangazwa matokeo
jumla ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi Tanzania, viongozi wa wilaya za
mkoa wa Songwe wameahidi kufanya vema katika mwaka ujao ili kuondokana na aibu
ya kuwa miongoni mwa mikoa 10 ya mwisho.
Ahadi hizo zilitolewa katika
ukumbi wa sekondari ya Vwawa wakati Kamati ya Mkoa ya Uendeshaji wa Mitihani ilipokuwa ikitoa matokeo jumla kwa viongozi wa Halmashauri zote tano za mkoa
huo.
Akisoma matokeo hayo Mwenyekiti
wa Kamati hiyo ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa huo Eliya Ntandu aliwambia
viongozi wa wilaya hizo kuwa mkoa wao umekuwa miongoni mwa mikoa 10 ambayo
haikufanya vizuri.
Aliongeza kuwa hali hiyo
imechangiwa na kufanya vibaya kwa kila wilaya ambako pia kulichangiwa na ufaulu
duni wa shule moja moja ambao unagusa wadau mbalimbali wa elimu.
Katika matokeo hayo Halmashauri ya Mji wa Tunduma imekuwa kinara, ikifuatiwa
na Mbozi, huku nafasi ya tatu ikikaliwa
na Ileje, ya nne Songwe na mkiani ipo wilaya ya Momba.
Shule ya binafsi ya Ilasi
imeonekana kufanya vizuri baada ya kutoa mwanafunzi wa kwanza kimkoa huku shule
ya msingi Kambarage ya Hamashauri ya Wilaya ya Songwe ikiwa haina mwanafunzi
hata mmoja atakayekwenda sekondari.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya
Wilaya ya Ileje Mh. Ubatizo Songa alitoa wito kwa Wanasongwe kutofurahia hali
hiyo na kuahidi kujipanga upya ili
kuachana na kuondokana hiyo.
Aliongeza kuwa,upya wa mkoa
kisiwe kisingizio cha kufanya mambo vibaya yanayoleta matokeo duni na kuuabisha
mkoa.
Kauli hiyo, iliungwa mkono na
Mwenyekiti Kamati ya Uendeshaji Mitihani
alipokuwa akifunga kika hicho alipowataka viongozi kwenda sehemu kwenye vituo
vyao vya kazi ili kubaini mapungufu yaliyojitokeza kna kuyatautia ufumbuzi
kulingana na mazingira ya kila halmashauri.
Mkoa wa Songwe ulianzishwa
mwanzoni mwa mwaka huu ukiwa umemegwa toka mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa mikoa
mipya ya Tanzania iliyoanzishwa miaka ya hivi karibuni hapa nchini,mikoa
mingine ni Njombe,Simiyu,Geita na
Katavi.
Viongozi wa mkoa wa wa Songwe wakijiandaa kutoa matokeo jumla ya mkoa ya Kumaliza Elimu ya Msingi 2016.
.Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe akitoa maagizo wakati wa kufunga kikao hicho
Kaimu Afisa Elimu wa mkoa wa Songwe akizungumza na wajumbe wa kikao hicho.
Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ileje akichangia
Mh. Mwenyeki wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje akiongea
Wajumbe toka Halmashauri ya wilaya ya Mbozi
Wajumbe toka Halmashauri ya Wilaya ya Momba
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni