Jumatatu, 23 Januari 2017
KANISA LA UWATA ISONGOLE WAPATA GARI
Maandamano barabarani wakifurahia watazamaji wakidhani
ni harusi
Wakitoa gari lililokuwa limetunzwa kwa mmoja wa
waumini wa UWATA
UWATA wakiwa barabarani kuelekea kwenye jengo lao
Jengo la zamani la Tawi la UWATA la Isongole-Ileje
Jengo jipya la UWATA la Isongole-Ileje
Alhamisi, 12 Januari 2017
ILEJE WAADHIMISHA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KWA KUPANDA MITI
Mkuu
wa Wilaya ya Ileje Mh.Joseph Mkude akielekea eneo la upandaji miti
Na;Daniel Mwambene, Ileje
Watumishi wa Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na wadau wengine
wilayani Ileje wamesherekea Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kupanda miti
ili kuilinda wilaya hiyo dhidi ya ukame.
Zoezi hilo lililoongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh.Joseph
Mkude pia lilihusisha watendaji wa ofisi yake, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Wakuu wa Idara na Vitengo, Wahudumu wa
Ofisi pamoja na wadau wengine
Katika zoezi hilo Zaidi ya miti 200 iliyonunuliwa na Ofisi
ya Mkurugenzi ilipandwa katika eneo la boma jipya lililopo mjini Itumba ambayo
ni makao makuu ya wilaya hiyo.
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo kukamilika Mkuu wa
Wilaya hiyo aliwataka watumishi kuwa na mwitikio chanya katika matukio kama
hayo akisema kuwa yanaashiria uzalendo kwa Taifa.
‘’Ndugu zangu watumishi nawashukuru kuitikia wito wangu lakini
naomba msichukulie matukio kama haya kuwa ni adhabu bali ni sehemu ya kazi
inayotakiwa kukuongezea furaha katika moyo wako’’,alilisisitiza Mh. Mkude.
Alisema kuwa miti mingi iliyopo katika maeneo
yanayotuzunguka haikufikia hapo bila juhudi za watu kufanyika kwa
kuipanda au kuitunza,tabia ambazo alisema haina budi kuenziwe kwa kupanda miti
kama zoezi lilivyofanyika.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw Haji Mnasi aliiahidi kusimama zoezi hilo
na kuwataka viongozi wa halmashauri kufanya ukaguzi wa kila sehemu
watakayotembelea ndani ya wilaya hiyo ili kujua utekeleji wa wa zoezu la upandaji miti
unavyokwenda.
Mnasi aliongeza kuwa ni wajibu wa kila kiongozi wa ngazi ya halmashauri hadi
kitongoji kuhakikisha anafuatilia zoezi hilo kwa walio chini yake na mwananchi
mmoja mmoja.
Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo Afande Fadhil Ishekazoba aliwataka
wananchi kulinda miti iliyopandwa ili kuepukana na kufanya kazi ambayo haina
matokeo chanya.
Alisema kuonesha kazi ilifanyika ni vema kuona ongezeko la
miti inayokuwa katika maeneo mbalimbali
badala ya kuwa na idadi kubwa ya miti inayopandwa kila mwaka huku
ikiishia kuliwa na mifugo pamoja na kuharibiwa na wanaokata kwaajili ya nishati
ya kupikia.
Akizungumza kwa niaba ya watumishi walioshiriki zoezi hilo
Afisa Elimu Msingi Mwalimu Godwin Mkaruka aliahidi kuongeza idadi ya miti
katika wilaya hiyo akitumia jeshi lake ambalo ni wanafunzi wakiongozwa na
walimu wao
Alisema kuwa kila shule ilishaandaa kitalu cha miche tangu
mwaka jana ukiwa ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Mkoa huu wa Songwe Mh.Chiku
Galawa aliyezitaka shule zote za msingi na sekondari kufanya hivyo.
Katibu
Tawala Wilaya ya Ileje Bi; Mary Joseph Marco akipanda mti
Mmoja
wa watumishi wa halmashauri akiwa kazini
Mkuu
wa Wilaya akipanda mti
Mkurugenzi
Mtendaji wa Wilaya ya Ileje Haji Mnasi akishiriki kupanda miti
Watumishi
wa serikali wakishiriki zoezi hilo
Washiriki
wa upandaji miti wakifurahia hotuba fupi ya Mkuu wa Wilaya
Mkuu
wa Polisi(OCD) wa Wilaya ya Ileje Afande Fadhil Majjid Ishekazoba akizungumza
na walioshiriki upandaji wa miti akisisiza kuitunza
Jumatatu, 9 Januari 2017
SERIKALI WILAYANI ILEJE YAHIMIZA UJENZI WA VYOO BORA
Wajumbe
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wakielekea kukagua choo cha wanafunzi shule ya
sekondari Nakalulu
Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mh. Joseph Mkude amewagiza viongozi
wa Serikali za Mitaa wilayani humo kuhakikisha wanasimamia vyema ujenzi wa vyoo
bora katika shule na kuondokana na ujenzi wa vyoo vya muda.
Alitoa maagizo hayo wakati akiongoza Kamati ya Ulinzi na
Usalama kukagua shughuli za ujenzi katika baadhi ya shule za sekondari ikiwa ni
siku moja kabla ya kuanza muhula wa kwanza wa masomo 2017.
Ziara hiyo ililenga katika kujiridhisha na maandalizi ya uwepo
na ubora wa vyoo,vyumba vya madarasa na matumizi sahihi ya fedha zinazotolewa
na serikali.
Mh.Mkude akizungumza kwa nyakati tofauti katika shule za
sekondari Itumba,Ileje,Nakalulu Kakoma na Mbebe alisikitishwa na hali aliyoiona
katika baadhi ya shule hizo katika vyoo vya walimu na wanafunzi akisema kuwa
haviendani na hadhi ya walimu.
Alisema kuwa vyoo vilivyopo katika shule za Nakalulu na
Kakoma havichochei walimu kupenda mazingira ya kazi na haviendani na viwango
vyao vya elimu ambayo ni mwanga kwa jamii inayozunguka shule.
‘’Vyoo vya shule vikiwa bora vinaweza kubadilisha ubora wa
vyoo katika jamii kwa vile wanafunzi wakihitimu wataiga ujenzi huo na kuboresha
zaidi na kabla ya mtu kuanza na ujenzi ya nyumba ya kuishi choo kiwe cha kwanza’’,alisema
Mh. Mkude.
Akizungumza katika sekondari ya Mbebe aliwataka madiwani
kuwatumia vema wataalam waliopo katika halmashauri hiyo kwenye masuala ya
ujenzi na manunuzi ili kuijengea heshima halmashauri hiyo.
Kauli hiyo pia ilifuatia kasoro alizozibaini kwenye manunuzi
ya mabati ya shule ya sekondari ya hiyo ambapo mabati 115 yalibainika kuwa
chini ya viwango vinavyotakiwa katika majengo ya serikali hali iliyosababisha
aagize yarudishwe kwa mwuzaji na kuchukua mabati yanayotakiwa.
Kwa upande wao, viongozi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo
walipongeza juhudi zinazofanywa na kiongozi huyo,katika usimamizi wa shughuli
za maendeleo kwa kufika maeneo husika bila kusubiri taarifa za mezani wakisema
watendaji wengine hawana budi kuunga mkono juhudi hizo.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, alimfananisha kiongozi huyo
na baadhi ya viongozi waliotangulia ambao ni aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo
marehemu Stivin Kibona, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya hiyo marehemu Luhonzyo Siwale pamoja
marehemu Mwangomo aliyekuwa Afisa Maliasili ambao alisema licha ya kuondoka
hapa duniani bado matunda ya kazi zao yanaonekana.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo
Mh.Gwalusako Kapesa alimpongeza Mkuu wa Wilaya kwa jinsi anavyokuwa wazi hali
aliyoielezea kuwa inaashiria ucha Mungu na ikifanywa na viongozi wengine
itajenga hali kuaminiana katika kazi.
Pamoja na mambo mengine Mkuu wa Wilaya aliwataka viongozi
wote kushirikiana katika kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kuanza
kidato cha kwanza wanafanya hivyo na kufuatilia kwa kina wale wanaosena wamekwenda
shule za binafsi badala ya zile za serikali.
Huku hali ikiwa mbaya kwa shule hizo kwa upnde wa vyoo bado
kuna shule zimenufaika na ujenzi wa vyoo bora kwa ufadhili wa SEDP ambazo ni
Luswisi,Itale,Msomba na Bupigu.
Vyoo
vya walimu na wanafunzi katika sekondari ya Kakoma kilichojengwa chini ya
viwango ambacho Mkuu wa Wilaya alikelezea kuwa kinadhalilisha watumishi wa Umma
Mkuu wa Wilaya ya Ileje (kulia) akipata maelezo toka kwa Afisa Mtendaji wa kata ya Mbebe Nickson Mwashitete (kushoto) kuhusu matumizi ya fedha zilizotolewa na Halmashauri kwa shule ya sekondari Mbebe
Mh.Mkude akiangalia ubora wa mabati kulingana na viwango vinavyotakiwa na serikali ambapo akisaidiwa na Mhandisi wa Ujenzi wa Wilaya alibaini mabati 115 yasiyokidhi viwango katika sekondari ya Mbebe.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje wakimsikiliza Mkuu Wilaya (hayupo pichani) ni ndani ya chumba cha darasa katika sekondari ya Mbebe.
Ijumaa, 6 Januari 2017
KAMATI YA ULINZI ILEJE KILA MMOJA KULEA MITI KUMI
Mto Itumba ulivyofurika hadi kwenye mashamba ya wakazi
wa kitongoji cha Kibanji katika kijiji cha Itumba
Na: Daniel Mwambene,Ileje
Katika kutimiza kwa vitendo zoezi la kila mwanafamilia
kupanda miti kumi, wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Ileje
mkoani Songwe kila mmoja amegawiwa miti kumi na kutakiwa kuwa mfano wa kuigwa
katika kuitunza.
Akigawa miche ya miti katika viwanja vya ofisi za wilaya
Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Joseph Mkude aliwataka wajumbe hao kuhakikisha kila
mmoja wao anapanda miche hiyo na kuilea ili iweze kukua na kufikia hatua nzuri.
“Tutakuwa tunakagua miti yenu kwanza kisha kwa Wakuu wa
Idara wote, Wah. Madiwani na wananchi wengine ambapo kila mwanafamilia anatakiwa
kupanda na kuilea naagiza kila kiongozi kwenye ngazi yake ahakikishe anasimamia
zoezi hilo”alisisitiza Mh,Mkude.
Katika mgao huo miche ya miti ya mbao,na kivuli iligawiwa
kwa wajumbe hao ikiwa imenunuliwa na ofisi yake huku viongozi wa
taasisi,makanisa na misikiti wakitakiwa kufanya hivyo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa miche hiyo Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo aliahidi kulinda miti hiyo sanjali na
kusimamia watendaji walio chini yake.
Huku hayo yakijili wakazi wa vitongoji vya Chafwonya na
Kibanji katika kijiji cha Itumba baadhi yao wameonja madhara ya kutoacha mita 60 toka kwenye mto
zilizopo kesheria baada ya Mto
Itumba kufurika kutokana na mvua zinazoendelea
kunyesha katika kata za Ndola na wilaya ya Mbeya Vijijini ambako ni chanzo cha
mto huo.
Uchunguzi wetu ulibaini mto huo kufurika hadi kwenye
mashamba ambayo yamegharimu wakulima maelfu ya fedha za mbolea za chumvi
chumvi.
Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mh.Joseph Mkude (kulia) akimgawia
miche Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Haji Mnasi (kulia)
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wakiwa na sehemu ya
miche waliyokabidhiwa na mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh Joseph Mkude.
Jumanne, 3 Januari 2017
KATIBU TAWALA MKOA WA SONGWE ATOA SOMO KWA WATUMISHI WA UMMA MKOANI SONGWE
Na Daniel Mwambene
Songwe
Watumishi wa umma mkoani Songwe wametakiwa kutulia katika vituo vyao vya kazi
ili kuwatumikia wananchi na kuwapunguzia gharama za
kuendesha familia zao.
Wito huo ulitolewa na Katibu
Tawala wa Mkoa wa Songwe Mh. Elia Tandu wakati alipokuwa akizungumza na Wakuu wa
Idara na vitengo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje
kwenye ukumbi wa Mkuu wa Wilaya hiyo akiwa katika ziara ya kikazi.
Mh. Tandu alisema kuwa kutotulia
katika vituo vya kazi siku za mwisho wa juma kwa baadhi ya watumishi hao kwa
kisingizio cha kusafiri kwenda kuona familia zao kuna athari kubwa kwa
serikali,wananchi na kwa maisha ya mtumishi mwenyewe.
Alisema kuwa limekuwa tatizo
kubwa kwa baadhi ya watumishi wa umma kusafiri nje ya wilaya zao na mkoa siku za
mwisho wa juma na sikukuu bila kufuata taratibu za kisheria hali inayosababisha
usumbufu kwa waajiri wao pindi wanapowahitaji katika kipindi hiki cha serikali
ya Awamu ya Tano yenye kauli mbiu “Hapa Kazi tu”.
Aliongeza kuwa huduma kwa
wananchi zinategemea sana uwepo wao wa karibu hivyo kukosekana kwao
kunawaongezea wananchi ugumu wa maisha.
Pia aliwaambia watumishi hao kuwa, kuwa mbali na familia zao kwa kisingizio cha mazingira magumu ya vituo vya kazi
kunawaongezea gharama za maisha ambazo hazina msingi wowote kwakuwa wanakuwa na
bajeti za familia mbili kwa wakati mmoja sawa na mwanaume mwenye mitala (wake
wawili).
Alisema kuwa kupangiwa katika
maeneo hayo hawana budi kujua kuwa wana jukumu la kuzibadilisha jamii
wanazozikuta badala ya kuendelea kulalamikia ugumu wa mazingira huku wao
wakitakiwa kuwasaidia wananchi kuwa chachu ya maendeleo.
Akifafanua zaidi alisema kuwa
mkoa wilaya nyingi za mkoa wa Songwe zina changamoto zinazotautiana hivyo
serikali iliwatuma kutumia taaluma zao kwa kusaidiana na wananchi kuzikabiri
changamoto hizo.
Aliongeza kuwa kwa mtumishi
yeyete kuwa na fikra za kuhama huwa kunamchelewesha kimaisha hali aliyoielezea
kuwa haina budi kuachwa kwa kuwa wamejikuta hawahami huku wakiwa wametumia
rasilimali nyingi katika kutafuta uhamisho huo.
Alisema kuwa kwa mtumishi yeyote
ili kulinda utulivu wa akili yake hana budi kukifanya kituo chake cha kazi kuwa
ni makazi yake ya kudumu hali itakayomwongezea ubunifu katika mambo
anayoyafanya kila siku.
Akizungumza na watumishi wa kada
mbalimbali katika wa halmashauri hiyo kwenye Ukumbi wa Mwala mjini Itumba
Katibu Tawala huyo aliwataka watumishi hao kuzingatia maadli ya utumishi wa
umma nakuepukana na vitendo vyote vinavyoweza kupunguza kasi ya utendaji wa
serikali ya awamu hii yenye kupigania maslahi ya wanyonge.
Alisema kuwa mshikamano baina ya
watumishi wa idara mbalimbali ni silaha itakayoupeleka mkoa wa Songwe mahali
panapotakiwa na taifa letu lenye kuijenga Tanzania ya viwanda.
Aliwataka watumishi wa mkoa wa
Songwe kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha mpito ambapo serikali inashughulikia
uhalali wa watumishi wa umma kwa kuondoa watumishi hewa na wenye vyeti vya
bandia (feki).
Kwa upande wao watumishi hao
waliomba serikali iharakishe mazoezi ya uhakiki wa watumishi ili wale wanaotaka
kuhama kwasababu za msingi waweze kufanya hivyo.
Mh. Elia Tandu akizungumza na watumishi kwenye Ukumbi wa Mwala uliopo shule ya sekondari ya Itumba
Watumishi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje wakimsikiliza Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe
kweny Ukumbi wa Mwala
VITUKO NDANI YA MTO SONGWE WILAYANI KYELA
Na;Daniel Mwambene Songwe
Waswahili
husema kuwa” Macho hayana pazia”haya yalinikuta siku chache zilizopita
nikielekea Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwila uliopo Ileje katika mkoa wa Songwe.
Macho
yangu pekee hayakutosha kuweza kuona na kutunza kumbukumbu za kudumu juu ya
mambo niliyoyaona katika safari ya kuelekea katika mgodi huo nililazimika
kutumia kamera ili kila kitu kisiweze kupotea nikisafiri masaa kadha kutoka
Itumbamakao makuu ya wilaya ya Ileje kwa kuzipita wilaya za Kyela na Rungwe na
kurudi tena Itumba.
Mzunguko
huo mrefu unawatesa Wanaileje wengi ambao hutaka kutembelea mgodi wao ama kwa
kutalii ,mafunzo au kwa kazi maalum kwasababu tu ya miundombinu mibovu
inayowalazimisha kupitia wilaya za Kyela na Rungwe, ambapo viongozi wa sasa wa
wilaya hiyo wamesema inatosha wakichukua hatua za ujenzi wa barabara kupitia
Ngulugulu na mkakati wa ujenzi wa daraja kule Landani.
Katika
safari hiyo yapo mengi niliyoyaona na kupata maelezo juu ya uwepo wake nikiamini
kwa pamoja tunaweza kuchukua hatua iwapo uwepo wake ni wa faida au hasara.Tafadahali fuatilia mfululizo wa picha
hizi na maelezo yake kwa ufupi.
Ni
kwenye kilele cha Mlima Kaburo barabara ya Ndembo-Ileje kwenda Kyela
Mmoja
wa wavamizi wa msitu wa mlima Kaburo alinashwa na kamera yetu akiwa kwenye
shughuli haramu ya uchomaji mkaa katika pori hilo
Uharibifu
unaofanywa na wavamizi wanaochoma mkaa mlima Kaburo kunapunguza miti ya asili
na kuharibu mandhari ya mlima huo
Baadhi
ya viongozi wa Halmashauri ya Walaya ya Ileje wakiwa ndani ya msitu wa Kaburo kuangalia usalama wake
Uharibifu
wa mazingira jinsi ulivyochangia kuharibu mandhari ya Mto Kiwila juhudi kubwa
zinahitajika ili kurejesha hali yake
Lori
aina ya Fuso (maarufu kama Mwalamusha) likipandisha Mlima Kaburo kutoka Kyela
kwenda Ileje
Waweza
kusema ni michezo ya kitoto katika maji kwa kutumia mashina ya migomba, hali haiko
hivyo inasemekana njia hiyo ni ya kusafirisha mbao katika Mto Songwe wilayani
Kyela mkoa wa Mbeya ambapo watu wazima huwatumia watoto kusafirisha mbao kwa
kufungwa pamoja na mashina ya migomba kama kiini macho ili kukwepa ushuru
pamoja na mkono wa serikali kwa ujumla
Upande
wa Malawi unavyoonekana katika mpaka wa Kasumulu (border) wilayani Kyela
Upande
wa Malawi unavyoonekana katika mpaka wa Kasumulu (border) wilayani Kyela
Biashara
ya maembe Busale-Kyela ambapo ndo moja ilikuwa ikiuzwa Tzsh.1000
Ramani ya mgodi wa Kiwila,mbele ni majengo ya utawala na kiwanda ,nyuma ni Mlima Kaburo ambao una zaidi ya tani milioni 30 za makaa ya mawe ambazo bado hazijachimbwa
Moja ya viberenge au treni zilizokuwa zikibeba makaa ya mawe kikiwa kwenye njia yake(reli)
Gari yaliyochakaa kwasababu ya kutelekezwa kutokana na kiwanda (mgodi) kusimama uzalishaji
Mlango wa kuingia ndani ya mgodi wa Kiwila
Moja ya mitambo iliyochakaa kutokana na kutofanya kazi kwa muda mrefu
Sehemu ya uzalishaji umeme katika mgodi wa Kiwila
Chumba cha kuongoza mitambo ya kuzalisha umeme mgodini hapo
Ndani ya karakana ya mgodi ambapo ilikuwa ikizalisha vipuli (spea) mbalimbali za mitambo
Jengo la utawa la katika mgodi wa Kiwila
Moja ya majengo maarufu sana mgodini hapo.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)