Mkuu
wa Wilaya ya Ileje Mh.Joseph Mkude akielekea eneo la upandaji miti
Na;Daniel Mwambene, Ileje
Watumishi wa Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na wadau wengine
wilayani Ileje wamesherekea Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kupanda miti
ili kuilinda wilaya hiyo dhidi ya ukame.
Zoezi hilo lililoongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Mh.Joseph
Mkude pia lilihusisha watendaji wa ofisi yake, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Wakuu wa Idara na Vitengo, Wahudumu wa
Ofisi pamoja na wadau wengine
Katika zoezi hilo Zaidi ya miti 200 iliyonunuliwa na Ofisi
ya Mkurugenzi ilipandwa katika eneo la boma jipya lililopo mjini Itumba ambayo
ni makao makuu ya wilaya hiyo.
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo kukamilika Mkuu wa
Wilaya hiyo aliwataka watumishi kuwa na mwitikio chanya katika matukio kama
hayo akisema kuwa yanaashiria uzalendo kwa Taifa.
‘’Ndugu zangu watumishi nawashukuru kuitikia wito wangu lakini
naomba msichukulie matukio kama haya kuwa ni adhabu bali ni sehemu ya kazi
inayotakiwa kukuongezea furaha katika moyo wako’’,alilisisitiza Mh. Mkude.
Alisema kuwa miti mingi iliyopo katika maeneo
yanayotuzunguka haikufikia hapo bila juhudi za watu kufanyika kwa
kuipanda au kuitunza,tabia ambazo alisema haina budi kuenziwe kwa kupanda miti
kama zoezi lilivyofanyika.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw Haji Mnasi aliiahidi kusimama zoezi hilo
na kuwataka viongozi wa halmashauri kufanya ukaguzi wa kila sehemu
watakayotembelea ndani ya wilaya hiyo ili kujua utekeleji wa wa zoezu la upandaji miti
unavyokwenda.
Mnasi aliongeza kuwa ni wajibu wa kila kiongozi wa ngazi ya halmashauri hadi
kitongoji kuhakikisha anafuatilia zoezi hilo kwa walio chini yake na mwananchi
mmoja mmoja.
Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo Afande Fadhil Ishekazoba aliwataka
wananchi kulinda miti iliyopandwa ili kuepukana na kufanya kazi ambayo haina
matokeo chanya.
Alisema kuonesha kazi ilifanyika ni vema kuona ongezeko la
miti inayokuwa katika maeneo mbalimbali
badala ya kuwa na idadi kubwa ya miti inayopandwa kila mwaka huku
ikiishia kuliwa na mifugo pamoja na kuharibiwa na wanaokata kwaajili ya nishati
ya kupikia.
Akizungumza kwa niaba ya watumishi walioshiriki zoezi hilo
Afisa Elimu Msingi Mwalimu Godwin Mkaruka aliahidi kuongeza idadi ya miti
katika wilaya hiyo akitumia jeshi lake ambalo ni wanafunzi wakiongozwa na
walimu wao
Alisema kuwa kila shule ilishaandaa kitalu cha miche tangu
mwaka jana ukiwa ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa Mkoa huu wa Songwe Mh.Chiku
Galawa aliyezitaka shule zote za msingi na sekondari kufanya hivyo.
Katibu
Tawala Wilaya ya Ileje Bi; Mary Joseph Marco akipanda mti
Mmoja
wa watumishi wa halmashauri akiwa kazini
Mkuu
wa Wilaya akipanda mti
Mkurugenzi
Mtendaji wa Wilaya ya Ileje Haji Mnasi akishiriki kupanda miti
Watumishi
wa serikali wakishiriki zoezi hilo
Washiriki
wa upandaji miti wakifurahia hotuba fupi ya Mkuu wa Wilaya
Mkuu
wa Polisi(OCD) wa Wilaya ya Ileje Afande Fadhil Majjid Ishekazoba akizungumza
na walioshiriki upandaji wa miti akisisiza kuitunza
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni