Na;Daniel Mwambene, Ileje - Songwe
Viongozi walioweka mifukoni
mwao SACCOS ya walimu Ileje watumbuliwa na uongozi wa mkoa wa
Songwe ili kuiokoa isitoweke katika ramani ya vyama vya ushirika hapa nchini.
Hatimaye sintofahamu na
kiza kinene kilichokuwa kinakikumba Chama cha Akiba na Mikopo cha Walimu
wilayani Ileje kwa takribani miaka miwili kimepata mwanga baada ya viongozi
waliokuwepo kuvuliwa madaraka kutokana na kanuni nyingi za uendeshaji kukiukwa
huku SACCOS hiyo ikiendeshwa kama mradi wa mtu asiyekuwa makini.
Kung’olewa kwao
kulitangazwa na Mrajisi wa Vyama vya Ushirika mkoani Songwe Marton Mtindya
kwenye mkutano maalum uliofanyika kwenye ukumbi wa Mkuu wa Wilaya hiyo mjini
Itumba ukiwaondoa mwenyekiti,katibu wake na baadhi ya wajumbe wa bodi kwa
kupoteza sifa za uongozi.
Walion’golewa ni mwenyekiti
Elimu Kaminyoge, katibu wake Alam Pwele na baadhi ya wajumbe wa bodi ambao kwa
muda wote walikuwa wakiendesha chama kinyume na sheria.
Akisoma taarifa kwa wajumbe
waliokuwa wamejaa jazba mlajisi wa mkoa huo Mtindya alitaja madhaifu kadha wa
kadha yaliyofanywa na viongozi hao na kuuelekeza ushirika huo katika kifo cha
milele wakisababisha watu kujiondoa uanachama kila uchapo badala ya kuongeza.
Mtindya aliyataja madhaifu
hayo kuwa ni kutochangia kila mwezi kama katiba yao inayoelekeza,kukopa pesa
bila kurejesha kila mwezi huku wengine kuwa na makato madogo tofauti na mkataba
wa mkopo, mwenyekiti na katibu kuandika barua za kujiondoa uanachama kwa
kupitishiana wao kwa wao katika makato ya shilingi 20,000/= ya kila mwezi
pasipo kushirikisha viongozi wengene huku wakiwa na mikopo mikubwa isiyo na
marejesho.
Alibainisha tuhuma zingine
kuwa ni kushindwa kuitisha mikutano mikuu kwa miaka miwili mfulululizo sasa
hali iliyosababisha wanachama kukosa taarifa za ushirika wao ambao ulikuwakimbilio
la wengi na kuwa ushirika wa kuigwa wilayani humo kwamiaka kadha iliyopita.
Aliongeza kuwa kutokana na
utendaji huo mbovu wastaafu,waliohama wilaya na waliojitoa uanachama SACCOS
imeshindwa kuwapa sitahiki zao ambazo walizitunza kwamalengo maalum ,hivyo
kuuchukulia ushirika kama sehemu ya utapeli
badala ya kuwa kimbilio,hali aliyoielezea kuwa haitavumliwa kwa SACCOS yoyote katika mkoa wa Songwe.
Mrajisi huo alipata wakati mgumu wakati wa kikao hicho kutokana na wanachama kuonesha hasira zao kwa viongozi wakieleza kutokuwa na imani nao kwa kutosikiliza shida zao kwa muda mrefu.
Pamoja na hali hiyo
kuchangiwa na viongozi hao Mtindya alieleza kuwa matatizo yalianzia kwenye
uongozi ulioondoka madarakani miaka miwili iliyopita ambapo walikuwa pia
wakitoa pesa kwa wanachama pasipo kufuata taratibu zinazotakiwa.
Licha ya kuvuliwa nafasi
zao za uongozi pia wametakiwa kujisalimisha kwa mwajiri wao ili kukubaliana ni
jinsi gani watalipa pesa wanazodaiwa ama sivyo ifikapo mwishoni mwa mwezi
Januari 2017 mishahara yao itazuiliwa kwa kile alichoeleza kuwa wamekenda
kinyume na ilani ya Chama Cha Mapinduzi inayolenga kuinua ushirika.
Said Ngondo mmmoja wa walionufaika na ukopeshaji huo haramu aliueleza mkutano kuwa nikwelikatika kipindi hicho alikopeshwa pesa posipo kujaza mkataba wowote ingawa kwa imani yake aliendeleakurejesha kila mwezi.
Mjumbe mwingine mwalimu
Alfred Mbukwa alinyoshea mkono pia baadhi ya watendaji wa Benki ya CRDB hasa
mtu aliyekuwepo katika mkutano wa mwisho 2014 aliyemtaja kwa jina moja la
Kayombo kuwa ana mchango wake katika kuifikisha pabaya SACCOS hiyo kwa vile
alionekana kutetea watuhumiwa pale walponyoshewa vidole kuwa walikuwa
wakiupeleka ushirika huo kusikojulikana.
Baada ya kuwang’oa vigogo
hao, uliundwa uongozi wa mpito ukiongozwa na mwalimu Damas Masebo aliyekuwa
Makamu Mwenyekiti, Said Ngondo akipewa umakamu Fabian Sigara akichukua nafasi ya
Meneja.
Wajumbe wengine wa bodi ni
Elias Bowa, Deogratius Mhume, Syoni Swila, Jose Songa na Lucian Yunga ambao kwa
pamoja wamepewa dhamana ya kuhakikisha ushirika huo unarudi kwenye mstari na
kuwa kimbilio la wengi.
Akizungumza mwishoni mwa
mkutano huo aliyeondolewa kwenye uenyekiti mwalimu Elimu Kaminyoge aliwaeleza
wajumbe kuwa hali hiyo ilichangiwa na hali mbaya aliyoikuta katika SACCOS ambapo
tayari lilikuwa ni pakacha lililokuwa likivuja.
Akizungumza nje ya ukumbi
huo, mmoja wa wajumbe wapya wa bodi hiyo mwalimu Deogratiuas Mhume alisema kuwa
katika wakati huu, viongozi hawana budi kuchukua maamuzi maguu na ya haraka ili
kuokoa watu wengi kama uongozi wa mkoa ulivyofanya ukishirikana na viongozi wa
serilkali wa wilaya ya Ileje.
Alisema kuwa kilichokuwa
ndani ya ushirika huo ni sawa na sumu ya nyoka ambaye dawa yake yaweza kuwa ni
kuondolewa kwa kiungo kilichofikiwa nasumu ili isienee mwili mzima.
Mrajisi
wa vyama vya ushirika mkoa wa Songwe Marton Mtindya (kulia) akituliza jazba
zilizowapanda wanachama, kulia kwake ni mwenyekiti aliyetemwa mwalimu Elimu
Kaminyoge
Mtindya
akielezea kwa wanachama mapungufu yaliyobainika katika ukaguzi uliofanyika
Mwalimu
Jose Songa akielezea jinsi viongozi wa SACCOS hiyo walivyochangia kuwaondolea
matumaini wanachama wake
Mwalimu
Alfred Mbukwa aliyesimama akielezea jinsi mmoja wa watumishi wa benki ya CRDB
alivyochangia kulinda uovu ndani ya ushirika huo
Sehemu
ya wanachama wa SACCOS hiyo wakiwa kwenye mkutano huo
Mwalimu
Syoni Swila aliyenyosha mkono akichangia katika mkutano huo
Mwalimu
Damas Masebo (maarufu kama Old Monkey) aliyepewa uenyekiti na kuhakikisha SACCOS
inarudi kwenye mstari akionyesha sura ya kazi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni