Mto Itumba ulivyofurika hadi kwenye mashamba ya wakazi
wa kitongoji cha Kibanji katika kijiji cha Itumba
Na: Daniel Mwambene,Ileje
Katika kutimiza kwa vitendo zoezi la kila mwanafamilia
kupanda miti kumi, wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Ileje
mkoani Songwe kila mmoja amegawiwa miti kumi na kutakiwa kuwa mfano wa kuigwa
katika kuitunza.
Akigawa miche ya miti katika viwanja vya ofisi za wilaya
Mkuu wa Wilaya hiyo Mh. Joseph Mkude aliwataka wajumbe hao kuhakikisha kila
mmoja wao anapanda miche hiyo na kuilea ili iweze kukua na kufikia hatua nzuri.
“Tutakuwa tunakagua miti yenu kwanza kisha kwa Wakuu wa
Idara wote, Wah. Madiwani na wananchi wengine ambapo kila mwanafamilia anatakiwa
kupanda na kuilea naagiza kila kiongozi kwenye ngazi yake ahakikishe anasimamia
zoezi hilo”alisisitiza Mh,Mkude.
Katika mgao huo miche ya miti ya mbao,na kivuli iligawiwa
kwa wajumbe hao ikiwa imenunuliwa na ofisi yake huku viongozi wa
taasisi,makanisa na misikiti wakitakiwa kufanya hivyo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa miche hiyo Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo aliahidi kulinda miti hiyo sanjali na
kusimamia watendaji walio chini yake.
Huku hayo yakijili wakazi wa vitongoji vya Chafwonya na
Kibanji katika kijiji cha Itumba baadhi yao wameonja madhara ya kutoacha mita 60 toka kwenye mto
zilizopo kesheria baada ya Mto
Itumba kufurika kutokana na mvua zinazoendelea
kunyesha katika kata za Ndola na wilaya ya Mbeya Vijijini ambako ni chanzo cha
mto huo.
Uchunguzi wetu ulibaini mto huo kufurika hadi kwenye
mashamba ambayo yamegharimu wakulima maelfu ya fedha za mbolea za chumvi
chumvi.
Mkuu wa Wilaya ya Ileje Mh.Joseph Mkude (kulia) akimgawia
miche Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Haji Mnasi (kulia)
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wakiwa na sehemu ya
miche waliyokabidhiwa na mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh Joseph Mkude.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni